Mheshimiwa Membe aliendelea kwa kusema kuwa ripoti ya umoja wa mataifa inathibitisha kuwa waasi wa M23 ni raia wa Rwanda.
M23 ni kikundi cha waasi walikuwa wakivunja amani na kuhatarisha usalama wa raia wa Kongo.
uhusiano wa Tanzania na Rwanda umekuwa matatani tangu rais wa Tanzania Dr:Kikwete kutoa ushauri kuwa serikali ya Kongo, Rwanda na Uganda wakae na kujadili jinsi ya kutatua mgogoro wa M23 kwa njia ya amani.
ushauri huu wa rais wa Tanzania ulipokelewa na matusi,kejeli na vitisho kutoka serikali ya Rwanda,ambapo serikali ya Rwanda ilifikia hata kuvunja baadhi ya mikataba ya kiuchumi wanayoshirikiana na Tanzania,
kwa upande wa pili, Tanzania iliendelea kusisitiza amani na kwamba haina kinyongo wala chuki na Rwanda, na kwamba itakuwa ni ya mwisho kuchukua hatua ikiwa itavamiwa.
Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) ndio liliongoza vikosi vya umoja wa mataifa katika Opareshen ya kuwatoa waasi wa M23 huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
28 Mei 2014 - 05:02
Msimbo wa Habari: 611788
Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Benard Membe ameliambia Bunge la Tanzania kuwa ana uhakika kuwa waasi M23 walitokea nchini Rwanda.