Jeshi la jamhuri ya kiislamu ya Iran limekamilisha matengenezo ya kombora jipya liitwalo Bavar-373.
kombora hili limesadikiwa kuwa na nguvu mithili ya kombola la S 300 ya Urusi. kombora hili lina uwezo wa kukinga mashambulizi ya anga ya adui ikiwemo mashambulizi ya ndege na makombora,ambapo huwa linakabiliana na hatari ya kombora au ndege ya adui kabla haijafikia lengo lake.
Ikumbukwe kuwa mnamo mwaka 2007 Iran alinunua kombora la S 300 kutoka kwa Urusi lakini haikukabidhiwa kombora hilo kutokana na mashinikizo ya Marekan na umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi.ndipo Iran ilipoamua kutengeneza kombora hilo bila ya kuhitaji msaada wa nje.
Iran imekuwa ikitengeneza makombora mengi ya masafa marefu ikiwemo Sayyad-2, Khalij-e-Fars (Persian Gulf), Mehrab (Altar), Ra’d (Thunder), Qader (Mighty), Nour (Light) and Zafar (Triumph) na mengineyo.
30 Agosti 2014 - 07:13
Msimbo wa Habari: 634432
Jeshi la jamhuri ya kiislamu ya Iran limekamilisha matengenezo ya kombora jipya liitwalo Bavar-373.