Shirika la habari AhlulBay (a.s) ABNA: imamu huyo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kongamano la kimataifa la maulama wa Kiislamu katika kuihami Palestina kuwa: misimamo ya wananchi wa Wapalestina si mambo ya ajabu kwa jamii ya Kiislamu, kwani manabii wa mwenyezi Mungu muda wote walikuwa wakipambana dhidi ya dhulma katika jamii za kibinadamu, ama katika karne hizi za karibuni serikali za kibeberu zimefanya juhudi mbali mbali ya kuisambaratisha hali ya kutetea na kupigania haki nakupinga dhulma, ama Imam Khomeini na mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameamsha hisia hiyo kwa Waislamu na walimwengu kwa ujumla na kufufua hisia ya kutetea haki za wanyonge duniani.
Sayyed Sadrud-dini Qabanchiy aliongeza kusema kuwa; kazi alioifanya Imam Khomeini na mabadiriko yaliofanyika katika zama hizi kupitia yeye imewapa wanyonge nguvu za kutetea haki zao katika mataifa mbali mbali, na kusisitiza kuwa muda wowote iwapo serikali zitafungamana na wananchi wake katika kutetea haki bilashaka wataifikia, na iwapo serikali haitakuwa tayari kuungana na wananchi basi wananchi wenyewe watajichukulia maamuzi ya kupambana dhidi ya dhulma na uonevu na hatimaye kuzipata haki zao.
Naye amebainisha kuwa: hivi sasa katika ukanda wa Gaza kuna wananchi wenye kauli mbio hii kuwa pamoja hatusaidiwi na serikali yetu bilashaka sisi haturudi nyuma hakika tutasimama kidete kuitetea haki zetu, aidha akisisitiza kuwa kile kinachojitokeza ukanda wa Gaza ni kufufua ushujaa kwa wananchi baada ya kuporwa ushujaa huo na serekali za kibeberu.
Imamu huyo akibainisha kuwa fitina ya Uislamu imedhihiri na vazi jipya alisema: maadui wa Uislamu wanatumia njia hiyo kutaka kuharibu Uislamu baina yetu Waislamu, hivyo basi wanazuoni wa Kiislamu wanapaswa kuwa makini katika kupambana na hali hiyo yakusambaratisha Uislamu.
Naye aliashiria hali halisi ya mazingira ya Iraq nakudhihirisha kuwa baada ya Iraq kuingia katika mabadiliko ya kisiasa, ambapo katika kipindi hicho tumepata ushindi ambao haukutarajiwa kupatikana kwa urahisi nchini, nao ni kuwaondoa wavamizi ndani ya nchi ya Iraq kwani lengo lao wavamizi hao ilikuwa ni kubaki daima katika nchi ya Iraq nakufanya mauaji ya kikatili, ama kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na serikali tumefanikiwa kuwatoa maadui hao.
Ushindi wa pili ni mshikamano uliotokea baina ya wananchi na jeshi katika kupambana na magaidi wa Daesh ambapo moja kati ya sehemu tulioshuhudia ushirikiano huo ni kuukomboa mji wa Amreli uliokuwa ukikaliwa na magaidi wa Daesh.
Mwisho alielezea jinsi walivyo ukomboa mji wa Amreli ambao wakazi wake ni Mashia kwakusema: mkoa wa Amreli kwa muda wa miezi mitatu ulikuwa umetekwa nakuwa chini ya magaidi wa Daesh, na magaidi hao hawakuwa wenye kuruhusu kuingiza hata kipande cha mkate katika mkoa huo kipindi chote hicho cha miezi mitatu, lakini wananchi wa Iraq wakishirikiana na jeshi la taifa wamefanikiwa kuukomboa mkoa huo, na hivi sasa tuko katika hatua ya mwisho ya kuwaondoa magaidi hao wa Daesh nchi Iraq kwa ujumla.