Matokeo ya awali ya kura ya maoni ya uhuru wa Scotland yamelewa ambapo wasiotaka kujitenga waongoza kwa kura.
Majimbo zaidi ya 20 yamekwisha toa matokeo huku wanaotaka kubaki chini ya himaya Uingereza wakiongoza kwa kupiga kura ya hapana kwa asilimia 55 dhidi 45.
Scotland imejiunga na Uingereza tangu miaka zaidi ya 300 iliyopita.Watetezi na wapinzani wa uhuru wamekuwa wakitetea misimamo yao hadi dakika ya mwisho.Wameitisha maandamano katika miji mikubwa ya kisiwa hicho.Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema ataendelea na wadhifa wake hata kama kura ya ndio itashinda. Wapinzani hata katika chama chake wanamkosoa kwa kudharau kwa muda mrefu vuguvugu la wanaotaka kujitenga.Hivi karibuni David Cameron ameahidi utwala mkubwa wa ndani kwa Scotland pindi wakiamua kuendelea na muungano.Matokeo ya kura hiyo ya maoni yanatarajiwa usiku wa leo kuamkia kesho.
19 Septemba 2014 - 07:21
Msimbo wa Habari: 638666
Matokeo ya awali ya kura ya maoni ya uhuru wa Scotland yamelewa ambapo wasiotaka kujitenga waongoza kwa kura.