Wanajeshi nchini Somali wameidhibiti jimbo na milima ya Galgala kutoka kwa wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab.
Milima ya Galgala imekuwa ngome ya Al-shabaab kwa miaka kadhaa wa kadhaa.
Kundi la Al-shabab ni tawi la kundi la Al-Qaeda na lina makao yake makuu kusini na katikati mwa somalia ambapo vikosi vya Umoja wa Afrika vinafanya mashambulizi dhidi ya kundi hilo.
Abdiweli Hirsi Abdille,ambaye ni waziri wa habari wa jimbo la kaskazini mashariki mwa Somalia Puntland amesema kuwa vikosi vya serikali vimeliteka jimbo hilo la Glagala katika mashambulizi yaliyojiri leo alfajiri.
1 Oktoba 2014 - 20:18
Msimbo wa Habari: 641723
Wanajeshi nchini Somali wameidhibiti jimbo na milima ya Galgala kutoka kwa wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab.