4 Oktoba 2014 - 18:12
Picha za Dua ya Arafa Iran

Siku ya Arafa ni siku muhimu sana kwa Mashia kwani ni mwanzo wa safari ya Imam Husein bin Ali bin Abitwalib, mjukuu wa mtume Muhammad s.a.w ambaye pia ni Imam wa pili wa Mashia ambaye aliuawa kikatili kwa kuchinjwa na kutenganishwa kichwa chake huko Karbala Iraq mnamo mwaka 62 Hijiria.

Leo ni siku ya tarehe 9 mwezi wa Dhulhaj 1433 Hirjia, siku ya leo ni maarufu kama siku ya Arafa ambapo mahujaj wakusanyika na kusimama katika jangwa la Arafa wakifanya ibada, kwa wale ambao hawajabahatika kwenda Hija huwa ni mustahabu kufunga na kufanya ibada katika siku hii. ambapo kesho itakuwa ni siku ya sikuu ya Eid al Adh-ha au Idi kubwa.
Iran ni moja kati ya nchi zenye idadi kubwa ya waislamu wa dhehebu la Shia Duniani, na inahesabika kuwa ni nchi pekee iliyosimamisha dola la kiislamu la dhehebu la Shia. Siku ya Arafa ni siku muhimu sana kwa Mashia kwani ni mwanzo wa safari ya Imam Husein bin Ali bin Abitwalib, mjukuu wa mtume Muhammad s.a.w ambaye pia ni Imam wa pili wa Mashia ambaye aliuawa kikatili kwa kuchinjwa na kutenganishwa kichwa chake huko Karbala Iraq mnamo mwaka 62 Hijiria.