Magaidi wa Daesh wameahidi kufanya mauaji ya halaiki katika mji wa Kuban ikiwa Marekani na washirika wake wataendeleza mashabulizi dhidi yao.
Magaidi hawa wa Daesh waliuteka mji wa Kuban siku ya Juma tatu baada ya mashambulizi makali biana yao na maaskari wa kikurd.
Umati mkubwa wa watu tayari umeondoka mjini humo na kuikimbilia Uturuki. Magari ya kuwabeba wagonjwa mahututi yameonekana yakiwabeba maelfu ya watu waliojeruhiwa katika vita vinavyoendelea kati ya Magaidi wa Daesh na Majeshi ya anga ya Marekani na washirika wake.
Milio ya mabomu,risasi na ndege za kivita vilikuwa vimetawala sauti zote za mji huo, inasadikiwa kuwa ikiwa Magaidi wa Daesh wanafanikiwa kudhibiti mji huu kikamilifu basi watakuwa wamethibiti sehem kubwa ya mipaka ya Sryria na Uturuki.
Umoja wa mataifa umeomba kulindwa haki za raia katika sehem hiyo.
7 Oktoba 2014 - 16:56
Msimbo wa Habari: 642841
Magaidi wa Daesh wameahidi kufanya mauaji ya halaiki katika mji wa Kuban ikiwa Marekani na washirika wake wataendeleza mashabulizi dhidi yao.