8 Oktoba 2014 - 19:23
Wakurd wa Syria wakabiliana vikali na Daesh

Wapiganaji wa Kikurdi wanakabiliana vikali na magaidi wa Daesh katika mji wa mpakani mwa Syria Kuban.

Wapiganaji wa Kikurdi wanakabiliana vikali na magaidi wa Daesh katika mji wa mpakani mwa Syria Kuban.
Sanjari na mashambulizi ya anga yanayofanywa na Marekani na Washirika wake, wanajeshi wa Kikurd wenye asili ya Syria wamefanya mashambulizi makali dhidi ya magaidi wa Daesh, wapambanaji wa kikurd wanafanya juhudi ya kuzuia mji wa Kuban usiingie mikononi mwa magaidi hao.
Yafaa kuashiria kwamba mji wa Kuban ni mji muhimu sana kwani upo mpakani mwa Syria na Uturuki na unahesabiwa kuwa magaidi na misaada inayokwenda kwa magaidi hao hupitia mipaka ya uturuki, hivyo wakiweza kuudhibiti mji huu itakuwa ni ushindi mkubwa kwao.

Tags