12 Oktoba 2014 - 16:37
Marekani: Mapambano dhidi ya Daesh ni shadidi sana

Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amesema kuwa: Mapambano dhidi ya magaidi wa Daesh ni shadidi na magumu mno.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amesema kuwa: Mapambano dhidi ya magaidi wa Daesh ni shadidi na magumu mno.
Hagel aliendelea kusema kuwa ingawa mashambulizi ya anga ya Marekani na washirika bado yanaendelea,hali bado ni tete na kunahitajika juhudi zaidi kukabiliana na magaidi hawa.
Vikosi vya wapiganaji wa Kikurdi wanaoulinda mji huo wameutaka muungano unaoogozwa na Marekani kuzidisha mashambulizi ya angani dhidi ya wapiganaji wa IS ambao wamezidi kuuzingira mji huo wa Syria uliyoko mpakani na Uturuki.
Wakati mapambano hayo yakiendelea huko Koban na kusababisha wahaka na hofu ya kutokea mauaji ya halaiki, uturuki imekataa kufungua mipaka yake ili wapiganaji wa kikurd wa Uturuki waliojitolea kupambana kuwasaidia wakurd wenzao wa Syria.
Wakurdi wa Uturuki wameahidi kuwa watawasha moto mkali na kusababisha machafuko ndani ya uturuki ikiwa uturuki haita wapa nafasi ya kwenda kuwasaidia wakurdi wenzao.
Katika hali ya kushangaza ni kwamba uturuki imekubaliana na Marekani kuendelea kuwafundisha magaidi mbinu za kijeshi ili waangushe serikali ya Syria.
Serikali ya Syria imekuwa ikishambuliwa na makundi ya magaidi toka nchi mbalimbali, makundi hayo ya magaidi yanaungwa mkono na Marekani na washirika wake na kupata udhamini wa wazi wazi kutoka kwa Saudia Arabia,Uturuki Qatar. kwa upande wa pili Serikali ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran imesimama kidete kuisaidia Serikali ya Syria kupambana na magaidi hao wa kimataifa.