Mkuu wa jeshi la Quds la Jamhuri ya kiislamu ya Iran amesema kuwa Marekani haita fanikiwa katika kupambana na magaidi wa Daesh huko Iraq na Syria.
Meja General Qasem Sulaimani: aliendelea kusema kuwa: Mahesabu ya Marekani katika kupambana na magaidi ni mahesabu yasiyo sahihi na kwamba hayataleta mafanikio.
Qasem Sulaiman aliendelea kubainisha kwamba: Marekani haitafanikiwa kuwaangamiza magaidi wa Daesh, pia Daesh haita fanikiwa kufikia malengo yake ya kutaa serikali za Iraq na Syria.
Yafaa kuashiria kwamba: Meja General Qasem Sulaimani ni moja kati ya majemedali na wataalamu wa mambo ya kijeshi ambao hawana mfano katika dunia, Qasema Sulaimani ndiye mkuu anayetoa mafunzo kwa jeshi la Hizbollah na jeshi la Syria.
Qasem Sulaiman amekuwa akitazamwa kwa jicho la pekee na serikali ya Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi kutokana na uwezo wake wa hali ya juu katika maswala ya vita.
20 Oktoba 2014 - 18:11
Msimbo wa Habari: 645673
Mkuu wa jeshi la Quds la Jamhuri ya kiislamu ya Iran amesema kuwa Marekani haita fanikiwa katika kupambana na magaidi wa Daesh huko Iraq na Syria.