3 Novemba 2014 - 20:25
Milipuko yaua mashia 34 wakiwa katika ziara

Sambaba na kutoweka amani katika maeneo mengi ya Iraq, kutokana na mauaji yanayofanywa na magaidi wa Daesh, pia kumeripotiwa milipuko kadha wa kadha katika sehemu mbali mbali za nchi hiyo.

Sambaba na kutoweka amani katika maeneo mengi ya Iraq, kutokana na mauaji yanayofanywa na magaidi wa Daesh, pia kumeripotiwa milipuko kadha wa kadha katika sehemu mbali mbali za nchi hiyo.
Mpaka sasa kumeripotiwa kuwa mashia 34 wamekufa kishahidi katika milipuko iliyolenga, mashia wanaokwenda Karbala kwa ajili ya kufanya ziara katika kaburi la Husein mjukuu wa mtume Muhammad s.a.w.
Yafaa kuashiria kwamba, waumini wa kiislamu wa dhehebu la Shia wamekuwa ni muhanga wa mabomu, ya maadui wa uislamu na maadui wa mtume Muhammad s,a,w ambao wanawaita mashia kuwa ni makafiri, na wanahamasisha watu kuwaua mashia kwa madai kwamba kuwaua mashia ni thawabu.