13 Novemba 2014 - 06:24
Viongozi Palestina  wakutana kujadili amani

Viongozi wa vyama vya FATIH na HAMAS katika Mamlaka ya Palestina wanakutana kwa mazungumzo, ili kupunguza wasiwasi wa kuvunjika kwa mpango wa maridhiano na amani nchini humo.

Viongozi wa vyama vya FATIH na HAMAS katika Mamlaka ya Palestina wanakutana kwa mazungumzo, ili kupunguza wasiwasi wa kuvunjika kwa mpango wa maridhiano na amani nchini humo.
Kikaohiki kimewekwa kufuatia matukio ya kuchomwa moto msikiti na vurugu za hapa na pale zinazoashiria kutokea mapigano makali kati ya utawala ghasibu wa Israel na waparestina.
Ikumbukwe kuwa siku ya juma tatu waisrael wawili waliuawa kwa kupigwa visu na vijana wanaosadikiwa kuwa ni waparestina, baada ya tukio hilo waisrael walichoma masjid na kutekeeteza kila kitu kilichomo ikiwemo vitabu vitukufu vya waislamu Qur an, jambo lililozua hasira kali kwa raia wa Parestina, na kusababisha vurugu za hapa na pale kuanza.
kikao hiki kimelenga kutafuta suluhisho la haraka kabla ya kuzuka vita kati ya pande mblili.
Vyama vya FATIH na HAMAS mnamo mwezi April mwaka huu, vilikubaliana kushirikiana na kutengeneza serikali ya pamoja ili kuendeleza taifa lao la Parestina.
Yafaa kuashiria kwamba Utawala wa Israel hauungi mkono umoja huo kati ya FATIH na HAMAS kwani unaitikadi kuwa Hamas ni chama cha magaidi kutokana na kwamba chama cha Hamas huwa kinajibu mashambulizi ya Israel kwa nguvu zote, hivyo kinaonekana kuwa ni tishio kubwa kwa utawala wa Israel.

Lebo