Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa karibu watu 1000 wameuawa nchini Ukraine tangu kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi Septemba. Tume ya Umoja huo kwa ajili ya haki za binadamu imesema utekelezwaji wa makubaliano hayo umekuwa wa kusuasua.
Ripoti hiyo imesema kwamba watu wengine zaidi ya 10,000 wamejeruhiwa katika vita hivyo ambavyo vimekuwa vikiendelea baina ya vikosi vya serikali na waasi wanaotaka kujitenga kwa sehemu ya mashariki mwa nchi hiyo. Wakati huo huo, Makamu wa Rais wa Marekani amewasili mjini Kiev, kushiriki katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuibuka kwa maandamani dhidi ya utawala wa wakati huo uliokuwa ukiegemea upande wa Urusi.
Waziri Mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk amesema anatarajia kwamba ziara ya bwana Biden itafuatiwa na tangazo la msaada zaidi kutoka Marekani, baada ya msaada wa Dola milioni 46 uliotolewa na nchi hiyo mwezi Septemba, kuimarisha usalama wa Ukraine.
21 Novemba 2014 - 10:29
Msimbo wa Habari: 652801
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa karibu watu 1000 wameuawa nchini Ukraine tangu kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi Septemba.