Serikali ya Urus imetoa onyo kali kwa Ufaransa kutokana na kuzuiliwa meli zake za kijeshi.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent fabius amesema leo kuwa mazingira kwa sasa si sahihi kuipatia Urusi meli ya kivita kutokana na mzozo wa Ukraine, wakati mbinyo unaongezeka kutoka Urusi kwa Ufaransa kukabidhi meli hiyo.
Serikali ya Urusi imesisitiza na kuionya Ufaransa kuwa inakabiliwa na matokeo mabaya hadi pale Ufaransa itakapokabidhi meli hiyo ya kwanza miongoni mwa meli mbili za kubebea helikopta za kijeshi zilizotakiwa kukabidhiwa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.
Lakini kutokana na mzozo wa Ukraine uliozuka katikati ya mwaka huu, Fabius amesema , nchi yake imekuwa katika mbinyo mkubwa kutoka kwa washirika wake , hususan Marekani , na imeahirisha hatua ya kuikabidhi Urusi meli hiyo mwezi Septemba mwaka huu.