7 Desemba 2014 - 09:36
Kimbunga chaleta maafa makubwa Ufilipino

Kimbunga kikali kimeleta dhoruba na maafa makubwa mashariki mwa Ufilipino.

Kimbunga kikali kimeleta dhoruba na maafa makubwa mashariki mwa Ufilipino.

Kimbunga hicho kijulikanancho kwa jina la Hagupit kimeshambulia maeneo ya mashariki na kati ya Ufilipino na kusababisha uharibifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kukatika umeme na kubomoa nyumba kadha wa kadhaa.

 Mamilioni ya watu wamekesha gizani usiku kucha wakati kukiwa na mvua kubwa na upepo unaovuma kwa kasi. Huduma za mawasiliano pia zimekatika katika baadhi ya maeneo yalioathirika wakati kimbunga hicho kikali cha Hagupit kikipiga mji wa pwani wa Dolores katika mkoa wa Samar Mashariki jana jioni. Mpaka sasa hakujawa na ripoti za mapema za vifo wala majeruhi lakini maafisa wanasema bado wanakusanya habari kutoka maeneo yaliyoathirika. Zaidi ya watu milioni moja wameyahama makazi yao na kutafuta hifadhi makanisani, shuleni na kumbi za umma katika mikoa 30. Maelfu ya watu wamekwama baada ya safari za angani na majini kusitishwa.

 

Lebo