Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, amesema hatua ya Ukraine kutaka kujiunga na Shirika la Kujihami la Mataifa ya Magharibi NATO inaleta kitisho kwa usalama wa Ulaya na kwamba mataifa ya Magharibi yanatumia juhudi hizo kama njia ya kuzichonganisha Urusi na Ukraine.
Hatua ya bunge la Ukraine kujitoa kwenye Jumuiya ya Mataifa Yasiyofungamana na Upande Wowote kama hatua ya kujiunga na NATO imeikasirisha Urusi na kuongeza mvutano kati ya Urusi na mataifa ya magharibi tangu kumalizika kwa vita baridi.
Lavrov ni kiongozi wa juu wa Urusi wa hivi karibuni kabisa kuzungumzia dhidi ya juhudi za Ukraine, na ambaye ameweka wazi kwamba Urusi utauona uanachama wa nchi hiyo kwa NATO kuwa mkakati wa jimbo hilo la zamani la iliyokuwa umoja wa Kisovieti kuwa ni kitisho cha moja kwa moja kijeshi.