Marekani hapo jana imewawekea vikwazo zaidi maafisa wa Korea Kaskazini na sekta ya ulinzi nchini humo kwa madai ya kuhusika na mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya kampuni ya kutengeneza filamu ya Sony Pictures, ambayo ilitengeneza filamu ya The Interview inayodhihaki na kudhalilisha serikali ya Korea Kaskazini.
Serikali ya Marekani inaunga mkono filamu hiyo onayodhihaki na kudhalilisha serikali ya Korea kaskazini, serikali ya Korea kaskazin haina mahusiano mazuri na Marekani kutokana na kutofautiana kimaslahi.
Ikulu ya Marekani imeonya kuwa hii ni moja ya hatua za wazi katika majibu ya Marekani kwa uchokozi uliofanywa na Korea Kaskazini. Huku vikwazo hivyo vikiwa na athari ndogo kwa kuwa tayari Korea Kaskazini inakabiliwa na vikwazo vingine ilivyowekewa na Marekani, kufuatia mpango wake wa nyuklia, Maafisa wa Marekani wamevieleza vikwazo hivyo kama vya kujibu tabia ya Korea Kaskazini iliovuka mipaka. Hata hivyo haijawahi kutokea kwamba Marekani inaweka vikwazo vya moja kwa moja kwa nchi yoyote ile kufuatia mashambulizi ya mtandaoni. Rais wa Marekani Barrack Obama amesema nchi hiyo bado inafikiria iwapo iirejeshe Korea Kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili shughuli za kigaidi. Hata hivyo Korea Kaskazini imekanusha kuhusika na shambulizi hilo la mtandaoni.