Waziri wa mambo ya kigeni wa jamhuri ya kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif amesema leo kwamba kuhusika zaidi kwa Urusi kunaweza kuharakisha mazungumzo yenye lengo la kufikia makubaliano muhimu juu ya mzozo unaohusisha mpango wake wa kinyuklia.
Wakati mkutano kati ya jamhuri ya kiislamu ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani ukianza tena mjini Geneva siku ya Jumatano, naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Ryabkov alikuwa akifanya ziara nchini Urusi, ambapo pande zote mbili zimeeleza nia yake ya kutaka kufikiwa makubaliano.
Wakati suala kuu ni kufikiwa makubaliano ya mwisho kabla ya muda wa mwisho wa Juni 30, mazungumzo hayo yamekwama kuhusiana na masuala muhimu.
Ryabkov , ambaye anaongoza ujumbe wa majadiliano wa Urusi chini ya mazungumzo ya mataifa matano pamoja na Ujerumani , amesema mahusiano mzuri kati ya jamhuri ya kiislamu ya Iran na Urusi unaweza kusaidia kufikiwa haraka kwa makubaliano ya kinyuklia na Iran.