19 Januari 2015 - 12:31
Waasi wapambana vikali na wanajeshi Yemen

Makubaliano ya kusitisha mapigano yamefikiwa nchini Yemen baada ya waasi wa Houthi na wanajeshi wa serikali kupambana vikali leo asubuhi katika mji mkuu Sanaa.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yamefikiwa nchini Yemen baada ya waasi wa Huthi na wanajeshi wa serikali kupambana vikali leo asubuhi katika mji mkuu Sanaa. Rais wa Yemen Abd Rabbu Mansour Hadi atakutana na washauri wake pamoja na maafisa wa kundi la waasi la Huthi kujadili masuala ya kisiasa na kikatiba. Waasi wa Huthi mapema leo asubuhi walikabiliana na wanajeshi karibu na ikulu ya Rais na kusababisha vifo kadhaa huku ving'ora vya magari ya kuwabeba wagonjwa vikisika vikilia kote katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa. Kilichochea mapambano hayo hakijabainika wazi huku kila upande ukiulaumu mwingine kwa uchokozi. Shule katika mji huo zimefungwa na familia nyingi zinasalia majumbani huku waasi wa Huthi wakishika doria mjini humo. Mapigano hayo yanakuja siku moja baada ya mnadhimu mkuu wa majeshi kutekwa nyara na waasi wa Huthi.