22 Januari 2015 - 19:56
 Urusi yalaani shambulizi dhidi ya basi Donetsk

Urusi imelilaani vikali shambulizi dhidi ya basi la abiria ambapo raia 13 wameuwa leo wakati basi walimokuwa wakisafiria liliposhambuliwa kwa makombora katika ngome ya waasi ya Donetsk mashariki mwa Ukraine

Urusi imelilaani vikali shambulizi dhidi ya basi la abiria ambapo raia 13 wameuwa leo wakati basi walimokuwa wakisafiria liliposhambuliwa kwa makombora katika ngome ya waasi ya Donetsk mashariki mwa Ukraine. Wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Urusi imevilaumu vikosi vya Ukraine kwa shambulizi hilo ikisema inalichukulia kama uhalifu dhidi ya ubinadamu na uchokozi wa wazi unaolenga kuvuruga juhudi za amani zinazofanywa kuutanzua mzozo wa Ukraine. Shambulizi hilo limefanyika saa chache baada ya mazungumzo ya amani mjini Berlin Ujerumani kutaka mapigano yasitishwe. Huku machafuko yakiendelea katika uwanja wa ndege wa Donetsk, jeshi la Ukraine limesema vikosi vyake vimeondoka kutoka eneo kubwa la uwanja huo katika siku mbaya kabisa ya vita vilivyodumu kwa muda wa miezi tisa.