23 Januari 2015 - 07:57
Mfalme wa Saudia arabia afariki dunia

Mfalme wa Saudi arabia Abdullah amefariki dunia mapema leo Ijumaa akiwa na umri wa miaka 91 na mdogo wake Salman atakuwa mfalme, ufalme wa nchi hiyo umeeleza katika taarifa.

Mfalme  wa  Saudi  arabia  Abdullah  amefariki  dunia  mapema  leo Ijumaa  akiwa  na  umri  wa  miaka  91 na  mdogo  wake  Salman atakuwa  mfalme, ufalme  wa  nchi  hiyo  umeeleza  katika  taarifa.

Mfalme  Salman  amemteua   ndugu  yake  wa  baba mmoja  Mugrin kuwa  mwanamfalme  na mfalme  mtarajiwa, akichukua  hatua  ya haraka  kuondoa  hofu  ya  mzozo  wa  kurithi  madaraka  katika wakati  huu  ambapo  Saudi  Arabia  inakabiliwa na  hali  ya mtafaruku  katika  mipaka  yake. 

Kuzuka  kwa  kundi  la  kigaidi la Daesh  nchini  Syria  na  Iraq kumesogeza  katika  mipaka  ya  nchi  hiyo  ya  Kifalme  kundi la wanamgambo  ambao  wameapa kuuangusha  utawala  wa  kifalme wa  Al Saudi.

Lebo