Waasi wa Nigeria wa kundi la Boko Haram wamewaachia huru mateka 190 waliokuwa wakiwazuia na kuwarejesha kijijini mwao katika jimbo la Yobe lililoko kaskazini mwa Nigeria. Mafisa wa jimbo hilo wamesema mateka hao waliachiwa huru kati ya siku ya Ijumaa na jana na bado mateka wengine wanazuiwa na waasi hao. Kiongozi wa kijiji cha Katarko amesema watu hao watawasilishwa kwa serikali hii leo ili kupokea misaada kwani nyumba zao zilichomwa wakati waasi hao wa Boko Haram walipokishambulia kijiji hicho. Msemaji wa Gavana wa jimbo la Yobe Abdullahi Bego amesema vijana, wanawake na watoto waliotekwa nyara tarehe sita mwezi huu, wameachiwa huru lakini kiasi ya watu wengine 20 bado wanazuiwa. Hayo yanakuja huku waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akitarajiwa kuwasili Nigeria hii leo ambako atakutana na Rais Goodluck Jonathan na kiongozi wa upinzani Muhammadu Buhari. Masuala yatakayojadiliwa ni kitisho cha Boko Haram na uchaguzi mkuu ujao.
25 Januari 2015 - 11:22
Msimbo wa Habari: 667020
Waasi wa Nigeria wa kundi la Boko Haram wamewaachia huru mateka 190 waliokuwa wakiwazuia na kuwarejesha kijijini mwao katika jimbo la Yobe lililoko kaskazini mwa Nigeria.