Afisa wa Serikali ya Israel amesema nchi hiyo haitaki kuendeleza mvutano kwenye mpaka wake na Lebanon, baada ya mapambano kati ya jeshi la nchi hiyo na wanamgambo wa Hizbullah, ambamo wanajeshi zaid ya 7 wa Israel waliuawa na wengine kujeruhiwa.
Afisa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, ametoa kauli hiyo katika mahojiano na Radio ya Israel, baada ya mkutano wa dharura wa maafisa wa usalama uliofanyika usiku mjini Tel Aviv. Mkutano huo uliodumu kwa saa kadhaa uliwahusisha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, waziri wa ulinzi Moshe Yaalon na kamanda mkuu wa jeshi la Israel Benny Gantz.
Ulifuatia shambulizi lililofanywa na kundi la Hizbullah la nchini Lebanon dhidi ya msafara wa jeshi la Israel, ndani ya eneo la mpaka ambalo ni sehemu ya Lebanon Isreal imelichukua kwa nguvu kutoka kwa Lebanon. Shambulizi hilo la Hizbullah liliwauwa wanajeshi wawili wa Israel wenye vyeo vya Kapteni na Sajenti, na kuwajeruhi wengine saba, hii ikiwa ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Israel Peter Lerner.
Lakini taarifa kutoka kwa wanajeshi wa Hizbullah zinasema kwamba wamewaua wanajeshi wasiopungua tisa, ambapo shambulizi hilo limeharibu magari ya jeshi la Israel takriban manne kwa kuyaangamiza kabisa.
Hizbullah ilikiri kufanya shambulizi, ambalo lilijibiwa na Israel kwa mizinga na mashambulizi ya anga ambayo hayakuipa hasara Hizbullah.
Shambulizi la Hizbullah kwa msafara wa kijeshi wa Israel ni shambulizi la kisasi baada ya jeshi la Israel kushambulia msafara wa Hizbullah aliyokuwa ukipambana na magaidi wa Syria na kuua watu saba ambapo askari wa Hizbullah walikuwa sita na mmoja alikuwa ni afisa wa ngazi za juu ya jeshi la Iran Jeneral Allah Dodii ambaye alikuwa akilisaidia jeshi la Syria kulipa mbinu za kijeshi kupambana na magaidi.
Netanyahu aonya kuhusu adhabu kali
Awali, Netanyahu alikuwa amesema waliolishambulia jeshi la nchi yake watalipa kwa gharama kubwa.
'Kwa wakati huu jeshi letu linashughulikia matukio kwenye mpaka wa kaskazini. Yeyote anayefikiria kutuchokoza kwenye mpaka huo, namshauri azingatie kilichotokea Gaza. Hamas ilipata kipigo kikubwa zaidi tangu kuundwa kwake, na jeshi letu liko tayari kujibu kwa nguvu kwenye mipaka yote''. Amesema Netanyahu.
Kwa upande wa Hizbullah ambayo iliishinda Israel katika vita vya mwaka 2006 na kulifanya jeshi la Israel kukimbia na kurudi nyuma katika uwanja wa mapambano, Imesema kuwa inasubiri Israel ifanye uendawazimu wa kuishambulia, ili iweze kuipa pigo litakalopelekea kusambaratika kabisa kwa taifa la Israel. Jeshi la Jamhuri ya kiislamu la Iran ambalo limepoteza askari wake wa ngazi za juu katika shambulizi lililofanya na Israel, limesema kuwa liko upande wa Hizbullah na litaisaidia Hizbullah kwa nguvu zote.
Jeshi la Iran ni linahesabika kuwa ni moja kati ya majeshi 10 yenye uwezo na nguvu za juu duniani.
Shambulizi la kisasi la Hizbullah limekuja siku kumi tu baada ya mashambulizi yanayo fanywa na Israel kuwauwa wapiganaji sita wa Hizbullah katika milima ya Golan Syria siku kumi zilizopita.
Mbali na wanajeshi wa Israel waliouawa au kujeruhiwa, mwanajeshi umoja wa mataifa raia wa Uhispania ambaye alikuwa katika ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo, pia alipigwa risasi na kuuawa na jeshi la Israel.
Balozi wa Uhispania kwenye Umoja wa Mataifa Roman Oyarzun Marchesi, amewaambia waandishi wa habari mjini New York, kuwa risasi iliyomuuwa mhispania huyo ilitoka upande wa Israel.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliitisha kikao cha dharura kuujadili mzozo huo, na rais wake wa sasa Cristian Barros Melet ambaye ni balozi wa Chile, amesema baraza hilo linalaani vikali shambulizi hilo la Israel lililomuuwa mwanajeshi wa kulinda amani.
Hata hivyo, licha ya karipio hilo kutoka baraza la usalama na katibu mkuu wa umoja wa mataifa mwenyewe, Ban Ki-moon, hakuna aliyethibitisha upande uliomuuwa mwanajeshi huyo lakini ishara zote zinaonyesha kuwa ameuawa na askari wa Israel ambao walichanganyikiwa baada ya kupata pigo kali kutoka kwa Hizbullah.
Stephane Dujarric ambaye ni msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema katibu mkuu huyo amesononeshwa na kuzorota kwa usalama kwenye mpaka baina ya Israel na Lebanon, na kuzitaka pande zote zinazohusika kuendeleza utulivu, na kuonyesha stahamala.
Hali hiyo ya mvutano imezifanya nchi hizo mbili kuzifunga shule zilizo karibu na mpaka, huku wakazi wa maeneo ya karibu na mpaka huo wakisema wamesikia milio milio ya silaha nzito.
Raia wengi wa Israel wamehama makazi yao,viwanja vya ndege vimefungwa na kumezuiliwa ndege za raia zisipae juu ya anga la Israel.
Ndege za kivita za Israel zimeonekana zikivuka mipaka na kuingia kwenye anga la Lebanon, jeshi la Hizbullah limesema ikiwa Israel itaanzisha vita basi hakuna sehemu ya Israel itakayo salimika, hivyo linawashauri wananchi waandae pakujificha, kwani litapiga makombora yasiyopungua elfu moja kila siku.
Israel imesema haitaki kupambana na Hizbullah hii ni ishara ya kutazama matokeo mabaya na athari inayotarajiwa kutokea katika vita hivyo.
Yafaa kuashiria kuwa hapo awali Israel ilipo shambulia askari wa Hizbullah na Iran ilionekana kujiamini na kujisifu kwa shambulizi ililofanya lakini baada ya jana Hizbullah kulipa kisasi jeshi la Israel na wanachi wake wanaona kwamba wameonewa kwa kulipwa kisasi kwa shambulizi hilo, ambalo Israel inasema kuwa ni shambulizi kali ambalo halijawahi kutokea katika msafara wake wa kijeshi.