Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls leo alijizuwia kuita China kuwa mshirika muaminifu wa Ufaransa, licha ya kuwa hilo lilikuwemo katika sehemu ya maandishi ya awali ya hotuba yake ambayo ilikwisha sambazwa kwa vyombo vya habari. Valls ambaye yuko katika siku ya pili ya ziara yake, aliyaondoa maneno hayo wakati akiipitia hotuba yake aliyoitoa baadaye kwa wafanya biashara mjini Beijing .
Badala yake alisema , Ufaransa na China ni mataifa mawili makubwa ambayo yanapenda kuzungumzia historia zao, utamaduni wao na misukosuko inayofungamana na uhuru wao.
Nchi hizo mbili ni wanachama wa kudumu wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifawenye kura ya turufu, ambapo China ni mshirika wa mara kwa mara wa Urusi katika kuyazuwia maazimio yanayoungwa mkono na nchi za magharibi.