25 Februari 2015 - 19:45
Jeshi la Iran lafanya luteka kubwa ya baharini + Picha

Jeshi la ulinzi wa mapinduzi la Iran leo limeanza luteka ya baharini katika mlango bahari wa Hormuz, kilomita karibu mia moja tu kutoka manuwari za nchi za magharibi, zinazohusika katika vita dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh lilipoegeshwa.

Jeshi la ulinzi wa mapinduzi la Iran leo limeanza luteka ya baharini katika mlango bahari   wa Hormuz, kilomita karibu mia moja tu  kutoka manuwari za  nchi za magharibi, zinazohusika katika  vita dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh lilipoegeshwa.

Vikosi vitatu vya  jeshi la utawala wa Iran vinashiriki katika luteka hiyo ya kawaida ya kijeshi, nje ya kisiwa cha Qeshm na  iliopewa jina la " Muhammad ni mtume mkuu ." Televisheni ya taifa imeonyesha shambulio la kombora la kisasa likifyatuliwa kutoka pwani. walinzi wa mapinduzi ndio wanaohusika na  ulinzi wa majeshi katika ghuba. majeshi ya majini yanakadiriwa kuwa  na karibu askari 20,000 wakiwa na  jukumu la kuzingira mlango bahari   wa  Hormuz pindi Iran ikishambulia. Mlango bahari  huo ndiko kunakopitia theluthi moja ya safari za meli zikiwemo zile za  mafuta.

Luteka hiyo ya  vikosi vya Iran inafanyika siku mbili baada ya manuwari  ya Ufaransa  ya kubebea ndege charles de Gaulle kuanza operesheni katika Ghuba, ikiwa ni sehemu ya  muungano unaopambana na kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq na Syria.

Luteka hii ya kijeshi ni luteka ya pekee kufanywa na majeshi ya ulinzi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, ambapo majeshi yameonyesha uwezo wake wa kijeshi wa hali ya juu, na kutoa ujumbe kwamba wako tayari kukabiliana na adui yeyote mwenye kuwa na mawazo potofu ya kuivamia jamhuri ya kiislamu ya Iran.

Iran ni nchi ya waajemi inayopakana na nchi za kiarabu, nchi za kiarabu zimepandikizwa chuki dhini ya Iran hivyo nchi nyingi za kiarabu kama Saudia Arabia zinaonyesha uadui wa dhahiri dhidi ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran. Iran ni nchi inayosifika kwa maendeleo ya katika nyanja mbalimbali ikiwemo sayansi na teknolojia na maendeleo katika sekta ya kijeshi na utengenezaji wa silaha za kisasa.