Jamhuri ya kiislamu ya Iran leo imetupilia mbali na kulipinga vikali pendekezo la rais Barack Obama kwamba nchi hiyo isitishe shughuli zake amani za kinyuklia kwa takriban miaka kumi, na kusema hilo halikubaliki. Msimamo wa Obama unaelezwa katika maelezo yasiyokubalika na ya kitisho, na Iran haitakubali madai ya kuvuka mipaka na yasiyo na mantiki.
Hata hivyo waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif amenukuliwa akisema kwamba nchi hiyo itaendelea na majadiliano ya kinyuklia na mataifa yenye nguvu duniani.
Katika mahojiano na shirika la habari la Reuters jana Jumatatu, Obama alisema Iran inapaswa kukubali kusitisha shughuli zake za kinyuklia kwa muda ambao unaweza kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu shughuli zake ili makubaliano yafikiwe kati yake na mataifa hayo yenye nguvu.
Serikali ya Marekani inaona kwamba nguvu za kijeshi za Iran, ni kikwazo kikubwa kwa Israel na kwamba zinahatarisha amani na usalama wa Israel.