Majeshi ya Iraq na wanamgambo wa Kishia wamepambana vikali na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu leo kusini mwa mji wa Tikrit unaoshikiliwa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh, licha ya kwamba mabomu ya kutegwa barabarani na mashambulizi ya kujitoa muhanga yamepunguza kasi yao ya kusonga mbele kuelekea katika mji huo.
Mapambano kuwania udhibiti wa mji wa Tikrit , mji muhimu katika mto Tigris yanaonyesha mafanikio makubwa kwa upande wajeshi la Iraq ambalo linapata msaada mkubwa kutoka kwa majeshi ya Iran, Tikrit umezungukwa kutoka maeneo matatu, kaskazini, magharibi na kusini, lakini kilichobakia ni upande wa mashariki tu. Waziri mkuu wa Iraq Haidar al-Abadi ametoa wito kwa raia kutendewa vyema.
Brigedia jenerali Saad Maan Ibrahim na msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wamesema kwa wataalamu wa mabomu wameweza kutegua mabomu mengi pamoja na mabomu yaliyotegwa ndani ya magari.