Pande mbili hasimu katika mgogoro wa nchini Libya zimeelezea matumaini kuhusu mazungumzo yanayofanyika kwa upatanishi na Umoja wa Mataifa nchini Morocco, yenye lengo la kupata muafaka wa kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Bernardino Leon ambaye alifanya mazungumzo na kila upande peke yake, wa wawakilishi wa mabunge hasimu ya Libya, amekiri kuwa bado kuna hali ya kutoelewana kuhusiana na majina yanayojadiliwa, lakini anataraji kuwa wawakilishi wa pande zote mbili wataweka kando tofauti zao na kufikia suluhu. Wakati huo huo, wanamgambo wenye silaha jana walikishambulia kisima cha mafuta cha al-Ghani nchini Libya, na kuwaua karibu walinzi wanane, ambapo waliwachinja baadhi yao, kabla ya majeshi ya eneo hilo kuwashambulia na kuchukua tena udhibiti wa kisima hicho cha mafuta.
7 Machi 2015 - 11:05
Msimbo wa Habari: 675232
Pande mbili hasimu katika mgogoro wa nchini Libya zimeelezea matumaini kuhusu mazungumzo yanayofanyika kwa upatanishi na Umoja wa Mataifa nchini Morocco