Shirika la habari AhluBayt (a.s) ABNA: mkuu wa masuala ya habari ya kijeshi nchini Ujerumani alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la (Volt Diego) la nchi hiyo ameashiria kunako kuweko baadhi ya wanajeshi waliokuwa na mitazamo potovu ya Daesh katika jeshi la Ujerumani nakulitaka jeshi kutowapa mafunzo yahali yajuu wanajeshi walikuwa na fikra hizo potovu.
Naye aliendelea kusema kuwa: kwamujibu wa uchunguzi uliofanyika katika jeshi hilo mpaka sasa watu 20 waliopewa mafinzo katika jeshi hilo wamejeunga na kikundi cha Daesh na huonekana nchini Syria wakiwa wanapigana upande wa Daesh.
Aidha alibainisha kuwa hivi sasa unafanyika uhakiki wa hali yajuu kabla ya mtu kujiunga na jeshi kwa kuchunguza familia anaetaka kujiunga na jeshi hilo ili kufahamu kuwa wanafungamano na vikundi vya kigaidi au la, ili kuepuka kutoa mafunzo kwa waliokuwa na fikra potovu ya kidaesh.
10 Machi 2015 - 18:10
Msimbo wa Habari: 675951
Kitengo cha masuala ya habari katika jeshi la Ujerumani kimetoa tahadhari ya kuwepo wanajeshi wenye fikra potovu ya Daesh katika jeshi la nchi hiyo