Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker ameonya juu ya kukosekana kwa maendeleo katika mazungumzo ya kuiokoa Ugiriki kutokana na hali mbaya ya kiuchumi, huku Ujerumani ikizusha uwezekano wa Ugiriki kujitoa kutoka kundi la nchi zinazotumia sarafu ya Euro. Juncker aliyasema hayo kabla ya mazungumzo yake jana na Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras ambaye chama chake cha mrengo wa kushoto Syriza kilishinda uchaguzi mwezi Januari. Kuna wasiwasi mkubwa kwamba Ugiriki itafilisika wakati wowote ule.Mwezi uliopita Ugiriki ilipata ridhaa ya kuongezewa muda wa mpango wa uokozi kwa miezi minne, licha ya Waziri Mkuu Tsipras kutamka hapo awali kwamba anataka kuachana na mpango wa hatua kali za kiuchumi na kutaka paweko na utaratibu mpya . Hata hivyo kumezuka mvutano mwengine kati ya Ugiriki na Ujerumani, baada ya Ugiriki kudai fidia ya deni linalotokana na mikopo iliyoipa Ujerumani wakati wa vita vya vikuu vya pili vya dunia. Mkosoaji mkubwa wa msimamo wa Ugiriki- waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schaueble ameonya kwamba muda unapotea na uwezekano wa kuitowa Ugiriki katika kundi la nchi zinazotumia euro, hauepukiki.
14 Machi 2015 - 20:56
Msimbo wa Habari: 676844
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker ameonya juu ya kukosekana kwa maendeleo katika mazungumzo ya kuiokoa Ugiriki kutokana na hali mbaya ya kiuchumi,