Milipuko miwili ya bomu imetokea leo karibu na kanisa moja la mjini Lahore, mashariki mwa Pakistan, wakati waumini wakikusanyika ndani, na kuwauwa watu kumi na nne. Naibu Mkuu wa Polisi wa Lahore Haider Ashraf amesema umati wa watu waliojaa hasira walimchoma moto hadi kufa mtu mmoja walioamini alihusika na shambulizi hilo na kujaribu kumuua mwingine. Amesema polisi wawili waliokuwa wakilinda kanisa hilo pia waliuawa katika miripuko hiyo. Takribani watu 80 wanaendeela kupatiwa matibabu hospitalini. Msemaji wa kundi moja lenye mahusiano na wanamgambo wa Taliban nchini Pakistan amedai kuhusika na shambulizi hilo akisema lilifanywa na walipuaji wawili wa kujitoa mhanga.
15 Machi 2015 - 19:22
Msimbo wa Habari: 677050
Milipuko miwili ya bomu imetokea leo karibu na kanisa moja la mjini Lahore, mashariki mwa Pakistan, wakati waumini wakikusanyika ndani