Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepata uungwaji mkono mkubwa kuunda serikali ya mseto. Msemaji wa ofisi ya rais ameliambia shirika la habari la AFP leo rais Reuven Rivlin anakamilisha mazungumzo ya siku mbili pamoja na wawakilishi wa vyama 10 vilivyoko bungeni kusikiliza nani wanaempendekeza kuwa waziri mkuu, ambapo vyama sita vimemuunga mkono Netanyahu.
Msemaji wa rais Jason Pearlman ameliambia shirika la habari la AFP amesema rais amekutana na hivi karibuni na chama cha Yisrael Beitenu na wamempendekeza Netanyahu na kufikisha jumla ya wabunge 67 miongoni mwa bunge lenye wabunge 120 ambao wanamuunga mkono kiongozi huyo wa Israel mwenye sera za kuendelea kuwadhulumu wapalestina ardhi na makazi yao.