Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri wa mambo ya nje wa Iraq (Dr Ibrahim Jaafari) katika maojiano maalumu na shirika la ABNA kuhusu msaada wa mshauri wa majeshi ya Iran katika kukabiliana na magaidi wa Daesh nchini Iraq amesema: sisi atushuulishwi na majina ya watu bali suala muhimju kwetu ni fungamano letu kisiasa na mataifa mingine.
Dr Ibrahim Jaafari alifafanua kuwa kila taifa litakalokuwa pamoja nasi, likatusadia misaada ya kibinadamu, nakutupatia ripoti muhimu, bilashaka tutamkaribi kwa heshima na taadhima katika taifa letu.
Aidha alibainisha kutokuwa na tufauti ya Daeshi kuweko Iraq au Syria alisema: kikundi cha kigaidi cha Daesh nitishio kwa watu wote duniani, kwa watoto, wakubwa, wazee, vijana na wanawake.
Waziri wa mambo ya nje wa Iraq pia aliisifu jamhuri ya kiislamu ya Iran kwakutoa msimamo wake haraka kuhusus jinai za Daesh nchini Iraq nakusema: jamhuri ya kiislamu ya Iran ilionyesha msimamo wake haraka katika kupambana dhidi ya Daesh, na katika mikoa mingi ya Iraq majeshi ya Iran yakopamoja na majeshi ya Iraq yakipambana na magaidi wa Daesh.
Pia alisema Iran ametusaidia hata tulipokuwa tunapambana na Daesh katika maeneo wanaoishi wakurdi nchini Iraq kitendo ambacho tunapaswa kuwapongeza.
Alipokuwa akijibu suali kuwa (nini mtazamo wako kuhusu athari ya kuwepo kamanda Qasim Sulaiman) kamanda wa jeshi la Quds la kulinda mapinduzi ya kiislamu nchini Iraq alisema: sisi tunaikaribisha Iran na shahsia zake zote katika kupambana na magaidi wa Daesh nchini Iraq.
23 Machi 2015 - 20:15
Msimbo wa Habari: 678617
Dr Ibrahim Jaafari amesisistiza kuwa: jamhuri ya kiislamu ya Iran imekuwa ikitoa msaada mkubwa katika kupambana na Daesh ambapo mikoa mingi nchini Iraq, wanajeshi wa Iran wakopamoja na waIraq wakipambana na magaidi wa Daesh.