Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya mambo ya ndani ya Morocco imetoa ujumbe unaashiria kuwatia mbalo magaidi 13 wa kikundi cha Daesh ambao walikuwa wakiandaa mazingira yakufanya vitendo vya kikagaidi vyakulipua shahsia muhimu za taifa hilo.
Abdulhaq Alkhayamu mchunguzi mkuu wa masuala ya kisheria nchini Morocco amebainisha kuwa lengo la kikundi hicho cha kigaidi ni kuunda utawala wa Daesh nchini humo ambapo wanachama hao waliokamatwa wako na umri wa miaka 18 na 34 ambao wakuwa wanajitaja kuwa niwajukuu wa Yusuf ibn Tashvyn, magaidi hao walikuwa na fungamano la karibu na viongozi wa Daesh walioko nchini Iraq na Syria.
Aidha amefafanua kuwa katika msako huo wamefanikiwa kukamata risasi 440, silaha 6 navifaa ya kutengezea mabomu, kompiuta moja pia pesa Dirham elfu 7 ambazo zimeingizwa kupitia nchi ya Ispania.
Morocco kuanzia mwaka 2002 mpaka sasa imesamparatisha vikundi vya kigaidi 132 nchini humo na kukamata magaidi elfu 2 na 720 pia kukamata kiasikikubwa cha silaha nchini humo.
24 Machi 2015 - 18:42
Msimbo wa Habari: 678779
Abdulhaq Alkhayamu amesema jeshi la ulinzi la nchi hiyo baada ya uchunguzi wa miezi mitano limefanikiwa kukamata wanachama 13 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh ambao walikuwa chini ya usimasimamizi wa mwananchi wa Morocco anaeishi katika mkoa wa Aghadir nchini humo