25 Machi 2015 - 18:39
Uchumi wa Palestina wazidi kushuka

Uamuzi wa Israel wa kuzuwia kiasi cha dola milioni 130 kwa mwezi katika mapato yaliyokusanywa kwa niaba ya mamlaka ya Palestina yanaubana uchumi wa nchi hiyo na kusababisha mfumo wa benki kutokuwa na fedha.

Uamuzi  wa  Israel  wa  kuzuwia  kiasi  cha  dola  milioni  130 kwa mwezi  katika  mapato  yaliyokusanywa  kwa  niaba  ya  mamlaka  ya Palestina   yanaubana  uchumi  wa  nchi  hiyo  na  kusababisha mfumo  wa  benki  kutokuwa  na  fedha.

Gavana  wa  benki  kuu  ya  Palestina   amesema  kwamba  Israel imesitisha  upelekaji  wa  fedha  hizo  za  kodi  na  ushuru  mwezi Januari  ikipinga  hatua  ya  Palestina  kujiunga  na  mahakama  ya kimataifa  ya  uhalifu  ifikapo   Aprili  mosi, wakati  mashtaka  ya uhalifu  wa  kivita  yatakapofikishwa  dhidi  ya  Israel, ambapo Israel iliivamia kijeshi Palestina na kufanya mauaji ya kinyama kwa muda wa siku 50 mutawaliya, watu wengi wasio na hatia waliuawa ambapo wengi wao ni wanawake na watoto mpaka sasa wengi wa wakazi wa palestina hawana sehem za kuishi wanaisi kwenye mapango na magofu.

Tangu  wakati  huo   zaidi  ya  dola  milioni 500 zimezuiwa  na  Israel , kuingia  katika  uchumi  wa  Palestina , na  kusababisha  mamlaka ya  Palestina , ambayo  inatawala  ukingo  wa  magharibi , kupunguza   mishahara  ya  wafanyakazi  wake  kwa  asilimia  40  na kuanza  kutumia  bajeti  ya  dharura.