Viongozi wa mataifa ya Kiarabu wamekubaliana katika mkutano wa kilele nchini Misri kuunda kikosi cha kijeshi cha pamoja kukabiliana na vitisho vinavyoongezeka katika kanda yao.
Viongozi wa mataifa ya Kiarabu wamekubaliana katika mkutano wa kilele uliofanyika Jumapili ya leo tarehe 29 mwezi wa 3 mwaka 2015, nchini Misri kuunda kikosi cha kijeshi cha pamoja kukabiliana na vitisho vinavyoongezeka katika kanda yao, ambavyo kwa madai yao ni vitisho vya kuongezeka utawala wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran.
Kwa mujibu wa azimio lililopitishwa na viongozi wa nchi hizo wawakilishi wa nchi za Kiarabu watakutana katika kipindi cha mwezi mmoja kutathmini uundaji wa kikosi hicho na kuwasilisha mapendekezo yao kwa mawaziri wa ulinzi katika kipindi kisichozidi miezi minne.
Rais Abdel Fatah al- Sisi wa Misri ameuambia mkutano huo wa kilele uliofanyika katika mji wa kitalii wa Sharm el - Sheikh kwamba ili kubeba dhamana kuu kutokana na changamoto kubwa zinazoyakabili mataifa hayo ya Kiarabu na kutishia uwezo wao,viongozi wa Kiarabu wamekubali kimsingi kuundwa kwa kikosi hicho cha jeshi la pamoja.
Kabla ya mkutano huo Mkuu wa Umoja wa Waarabu Nabil al- Arabi amesema uamuzi huo umechukuliwa kwa kiasi kikubwa ukiwa umekusudia kupambana na makundi ya kigaidi ya waislamu wa Sunii wanaodai kuwa ni wapiganaji wa jihadi ambao wamevamia sehemu za ardhi nchini Iraq na Syria na pia kujipenyeza nchini Libya.
Kundi la Daesh ni tishio
Mkuu wa Umoja wa Waarabu Nabil al- Arabi ameuambia mkutano huo wa kilele Jumapili kwamba eneo hilo linatishiwa na kundi la uharibifu ambalo linatishia uwepo wa dini na makabila mbali mbali yakiishi kwa pamoja na kwa amani,moja kwa moja alikuwa akilikusudia kundi la kigaidi la wapiganaji wa jihadi wa kisunni la Daesh ambalo lilikuwa likipokea udhamini na msaada kutoka kwa Saudia arabia kabla ya kundi hilo kuigeuka Saudia arabia na kutangaza vita dhidi ya yake na vibaraka wake, jambo lililopelekea Marekani na nchi za kiarabu kutengeneza jeshi kwa ajili ya kukabiliana na kundi hilo kabla halijaanza kuwa hatari kwa wadhamini wake.
Mkuu wa Umoja wa Waarabu Nabil al- Arabi amekaririwa akisema "kilicho muhimu leo ni kupitishwa kwa uamuzi huo muhimu kutokan na msukosuko unaoathiri ulimwengu wa nchi za Kiarabu."
Misri ilikuwa ikishinikiza kuundwa kwa kikosi cha kukabiliana na hali ya dharura kitakachoweza kupambana na wanamgambo kwa haraka na suala hilo likazidi kwa la dharura wiki hii baada ya Saudi Arabia na washirika wa nchi za Kiarabu kuanzisha mashambulizi dhidi ya wanamapinduzi wa kishia wa jamii ya Huthi nchini Yemen.
Arabi amesema mashambulizi hayo yataendelea hadi hapo wanamapinduzi wa kishia watakapoondoka katika maeneo waliyoyateka na kusalimisha silaha zao.
Nchi za kiarabu zinafanya hayo ili kuwalazimisha raia wa Yemen kumkubali rais Abedrabbo Mansour Hadi, ambaye raia wengi hampendi kutokana na kuwa kibaraka wa Israel, Marekani na Saudia arabia.
Mashambulizi dhidi ya raia wa Yemen yaendelea
Nchi kadhaa za Kiarabu ikiwemo Misri zinashiriki kijeshi katika mashambulizi hayo ambayo Mfalme Salman wa Saudi Arabia amesema hapo Jumamosi kwamba mashambulizi dhidi ya Yemen yataendelea hadi hapo wananchi wa Yemen watakapomkubali rais Abedrabbo Mansour Hadi.
Rais wa Yemen Abedrabbo Mansour Hadi mwanzoni mwa mkutano huo ametowa wito wa kukomeshwa kwa mashambulizi hayo pale tu wananchi wa Yemen na wanamapinduzi wa kishia Huthi watakaposalimu amri na kumrudia yeye madarakin, rais huyo wa Yemen ambaye hapo awali alijiuzuru na kisha kutangaza kujirudisha madarakani amemwita kiongozi wa wanamapinduzi wa kishia wa Huthi kuwa kibaraka wa jamhuri ya kiislam ya Iran.
Hata hivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amewataka viongozi hao wa Kiarabu kutafuta suluhisho la amani kwa mzozo huo wa Yemen.
Licha ya kuungwa mkono kwa uundaji wa kikosi hicho cha cha pamoja cha Waarabu bado itachukuwa miezi mingi kukiunda na baadae kufanya kazi kwa misingi rasmi.
Sisi amesema katika mahojiano ya hivi karibuni kwamba pendekezo la kuunda kikosi hicho cha pamoja limekaribishwa hususan na Jordan ambayo yumkini ikashiriki pamoja na Saudi Arabia,Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait wakiongozwa na Israel na Marekani katika mashambulizi dhidi ya Yemen.
Marekani yaahidi kuchangia kwa uwezo wake katika mapambano dhidi ya Yemen
Aaron Reese naibu mkurugenzi wa utafiti katika Taasisi ilioko Washington Marekani ya Masomo ya Vita amesema kila mmoja ya nchi hizo itachangia kwa uwezo tafauti ilio nao.
Wajordan wanajulikana kwa uwezo walio nao vikosi vyao maalum wakati Misri inatambulika kwa kuwa na jeshi kubwa na makambi karibu na Libya.
Misri ilikuwa ikitaka uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa kuingilia kati nchini Libya na kutupilia mbali jaribio la mazungumzo ya amani kwa jirani yake huyo wa Afrika kaskazini kuwa hayafai.
Mchakato wa amani wa Israel na Wapalestina kama ilivyo katika kila mkutano wa kilele wa Umoja wa Waarabu pia ulitajwa kwenye agenda na masuala mengine yaliyopewa pia kipau mbele ni kupambana na Kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq na Syria na mzozo wa Libya.


















