29 Machi 2015 - 19:03
Mtuhumiwa ugaidi auawa Tunisia

Waziri Mkuu wa Tunisia Habib Essid leo hii amesema mtuhumiwa mkuu wa shambulizi la kigaidi lililosababisha mauwaji ya watalii wa mataifa ya kigeni nchini humo ameuwawa katika operesheni ya kukabiliana na ugaidi.

Waziri Mkuu wa Tunisia Habib Essid leo hii amesema mtuhumiwa mkuu wa shambulizi la kigaidi lililosababisha mauwaji ya watalii wa mataifa ya kigeni nchini humo ameuwawa katika operesheni ya kukabiliana na ugaidi. Kauli hiyo ameitoa wakati maelfu ya raia wa taifa hilo wakiwa wameandamana katika maeneo yote ya mji mkuu kwa lengo la kukemea vikali vurugu zinazosababishwa na wenye itikadi kali. Shirika la habari la Tunisia limemnukuu waziri mkuu huyo akimtaja Khaled Chaieb, ambae vilevile anajulikana kama Abou Sakhr Lokman kwamba ameuwawa katika operesheni ya usiku uliopita katika mkoa wa Gafsa uliyo karibu wa mpaka wa Algeria. Chaieb inaaminika kuwa ni mpiganaji maarufu katika tawi la al-Qaeda kwa upande wa Afrika ya Kaskazini, na anatuhumiwa kuongoza au kusaidia shambulio la Machi 18 ambapo watalii 20 waliuwawa nchini humo.

Waumini wa kiislamu wa dhehebu la Sunni wamekuwa wakilaumiwa na kutuhumiwa kwa tuhuma za ugaidi katika maeneo mbali mbali duniani.