Rais mteule wa Nigeria Muhammadu Buhari ameapa leo kwa atachukua hatua kali dhidi ya kundi la Boko Haram na kuahidi kufanya maridhiano na kuunda serikali itakayojumuisha watu wa maeneo yote nchini humo katika hotuba yake ya kwanza tangu kushinda uchaguzi.
Buhari amesema huu ni wakati wa kuponya machungu , na kuongeza kwamba Wanigeria wameweka kando taifa la chama kimoja na kukumbatia demokrasia.
Wakati huo huo rais wa Barack Obama wa Marekani amemsifu rais Goodluck Jonathan leo kwa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa rais ambao amesema umeonesha nia ya Nigeria kutekeleza misingi ya demokrasia.
Obama amesema katika taarifa kwamba rais Jonathan ameweka maslahi ya taifa lake kwanza kwa kukubali kushindwa katika uchaguzi na kumpongeza rais mteule Muhammadu Buhari kwa ushindi.
Nae katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon nae amempongeza rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari kwa ushindi wake na kusema kwamba uchaguzi huo ni ushahidi wa ukomavu katika demokrasia nchini Nigeria.