3 Aprili 2015 - 18:09
 Pakistan yawahamisha raia wake Yemen

Bunge la Pakistan litakutana jumatatu ijayo kujadili kama wajiunge na opereshini hizo za kijeshi zinazoongozwa na Saudia arabia au la.Serikali mjini Islamabad imesema iko tayari kuihami na kuisaidia serikali ya Saudia arabia lakini haitaki kupalilia mgawanyiko wa kidini na kuwashambulia waislamu wa Yemen wasio na hatia.

Pakistan imewahamisha raia wake wasiopungua 200 hii leo kutoka Yemen katika wakati ambapo waziri mkuu Nawaz Shariff amekuwa na mazungumzo pamoja na kiongozi mwenzake wa Uturuki Ahmed Davutoglu. Pakistan haijajibu bado maombi ya Riyadh ya kujiunga na opereshini za nchi shirika dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Yemen, wanaompinga wa Yemen aliyetoroka nchi hiyo na kukimbilia Saudia arabia.

Bunge la Pakistan litakutana jumatatu ijayo kujadili kama wajiunge na opereshini hizo za kijeshi zinazoongozwa na Saudia arabia au la.Serikali mjini Islamabad imesema iko tayari kuihami na kuisaidia serikali ya Saudia arabia lakini haitaki kupalilia mgawanyiko wa kidini na kuwashambulia waislamu wa Yemen wasio na hatia.

Akizungumza nchini Uturuki baada ya mkutano wake pamoja na waziri mkuu Ahmed Davutoglu, waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Shariff amezihimiza pande zinazohusika na mzozo wa Yemen zijitahidi kusaka ufumbuzi kwa njia ya amani.