Raia wa Uholanzi ambae alitekwa nyara karibu miezi minne iliyopita na mtandao wa kigaidi wa AQIM, huko Timbuktu kaskazini mwa Mali amekombolewa leo katika operesheni za kijeshi za Ufaransa. Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema mateka Sjaak Rijke, ambae alitekwa tarehe 25 Novemba mwaka 2011 amekombolewa baada ya kufanyika operesheni ya kikosi maalum cha kijeshi ya taifa hilo.
Taarifa hiyo inasema operesheni hiyo vilevile imefanikisha kutiwa mbaroni kwa watu wengine kadhaa. Watu wenye silaha walishambulia hoteli ambayo Rijke alikuwa anaishi na kumkamata yeye na watu wengine kutoka Afrika Kusini na Sweden ambao wote hao bado wanashikiliwa mateka hadi sasa. Novemba 2014 mtandao wa kigaidi a AQIM ulitoa mkanda wa video ambao unaonyesha Rijke akitowa taarifa katika siku 1,000 tangu kushikiliwa mateka.