8 Aprili 2015 - 13:57
Ujerumani haitalipa fidia kwa Ugiriki

Ujerumani kwa mara nyingine tena imetupilia mbali miito kutoka Ugiriki kutakiwa kulipa mabilioni ya euro ikiwa ni fidia kutokana na vita vikuu vya dunia.

Ujerumani kwa  mara  nyingine  tena imetupilia  mbali  miito  kutoka Ugiriki  kutakiwa  kulipa  mabilioni  ya  euro  ikiwa  ni  fidia  kutokana na  vita  vikuu vya  dunia.

Ugiriki  imesema  siku  ya  Jumatatu  kuwa  Ujerumani  inapaswa kulipa zaidi  ya  euro  bilioni 278  baada  ya  utawala  wa  wanazi  wa Ujerumani  kuikalia  nchi  hiyo  kimabavu  kwa  muda  wa  miaka minne.

Naibu  kansela  Zigmar Gabriel  amekataa  wito  huo, akionya kwamba  Ugiriki  inachanganya madai  hayo  na  majadiliano yanayoiendelea  hivi  sasa  ya  kuuokoa   uchumi  wa  nchi  hiyo.

Gabriel  amewaambia  waandishi  habari  mjini  Berlin  jana  kwamba masuala  hayo  mawili  hayana  uhusiano  kabisa.