Shambulizi la anga lililofanywa na muungano wa majeshi ya nchi za ghuba zikiongozwa na Saudi Arabia kwa kuungwa mkono na Marekani limewaua watu 12 wasio na hatia siku ya leo katika mji wa kusini mwa Yemen wa Aden. Shambulizi hilo lililofanyika mapema leo alfajiri limelenga kambi ya kijeshi ya Al Dhahra kusini mwa jimbo la Taez na pia limewajeruhi wanaharakati wa kishia wa Huthi wanane. Kambi hiyo ni ya kikosi cha wanajeshi watiifu kwa aliyekuwa Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh.
Serikali ya Saudi Arabia imesema imefanya mashambulizi ya anga 1,200 tangu ilipoanzisha kampeni ya kuwalazimisha wananchi wa Yemen wakiongozwa na kikundi cha wanaharakati wa kishia wa Huthi kumkubali rais Hadi ambaye wananchi wa Yemen hawamtaki.
Mashambulizi hayo yaliyoanza tarehe 26 mwezi uliopita na yameua wananchi wasio na hatia zaidi ya 100.
Wanaharakati wa kishia wa Huthi wanaendeleza mapambano makali dhidi ya wanajeshi watiifu kwa Rais wa Yemen Abed Rabbo Mansour Hadi ambao wanasaidiwa na majeshi ya Saudia arabia na vikundi vya kigaidi vya Daesh na Al-qaida katika harakati ya kulidhibiti jimbo la Mareb lenye utajiri wa mafuta.
Amiri jeshi mkuu wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran Ayatollah Sayyed Ali Khamenei, ameionya Saudia arabia iache kuua wananchi wa Yemen na ameonya kuwa katika vita hivyo Saudia arabia na washirika wake watashindwa.
Marekani na Israel wako bega kwa bega na Saudia arabia katika mashambulizi dhidi ya raia wa Yemen, ambapo Jamhuri ya kiislam ya Iran iko upande wa wananchi madhulumu wa Yemen.