Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton, amezindua kampeni yake ya kugombea kiti cha urais nchini Marekani mwaka ujao kupitia chama cha Democratic. Mke huyo wa rais wa zamani Bill Clinton, alitoa tangazo hilo kupitia mtandao wake wa Twitter, pamoja na ukanda mfupi wa video kwenye tovuti yake Jumapili mchana, ambapo alijitanabahisha kama kinara wa mmarekani wa kawaida. "Nagombea urais. Wamerekani wamepambana kutoka katika nyakati ngumu za kiuchumi, lakini hali iliyopo bado inaendelea kuwanufaisha wale walioko juu. Wamarekani wa kawaida wanahitaji kinara, na nahitaji kuwa kinara huyo. Kwa sababu familia zikiwa imara, Marekani inakuwa imara," alisema katika ujumbe wake wa video. Clinton atalitembelea jimbo muhimu lenye maamuzi la Iowa kesho Jumanne na Jumatano, katika ziara yake ya kwanza ya kampeni.
13 Aprili 2015 - 08:46
Msimbo wa Habari: 683266
Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton, amezindua kampeni yake ya kugombea kiti cha urais nchini Marekani mwaka ujao kupitia chama cha Democratic