Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza kuipatia Iraq msaada wa ziada wa kiutu kiasi ya dola milioni 200. Rais huyo hata hivyo hakusema iwapo utawala wake utatoa helikopta chapa Apache pamoja na silaha nyingine kwa Iraq.
Obama ameweka wazi kwamba msaada huo utapitia katika serikali ya Iraq.
Rais Barack Obama amesema wakati nchi yake inafanya kazi pamoja na mshirika imara , kama Iraq ni muhimu kwa nchi hizo kuratibu shughuli zao ili hisia zisiwe kwamba Marekani inaelekea kurejea tena Iraq lakini Marekani inafanya kile ambacho ni muhimu kwa watu wa Iraq hata kama ni kujiunga na mapigano dhidi ya adui wa pamoja wa nchi hizo.
Marekani inaonekana kutofurahishwa na uwepo wa wataalam wa vita wa Iran nchini Iraq, ambapo wataalam hao wanasifiwa kuwa ndio wamesababisha jeshi la Iraq lipate mafanikio katika mapambano yake dhidi ya magaidi.