15 Aprili 2015 - 11:57
Vikwazo vya silaha dhidi ya wanamapinduzi wa Huthi

Weledi wa mambo wamestaajabishwa na kuwekwa vikwazo hivyo kwa wahuthi badala ya kuwekewa Saudia arabia ambayo imeivamia Yemen na kuishambulia kwa silaha nzito.

Baraza  la  usalama  la  Umoja  wa  Mataifa  limepitisha  azimio linaloweka  vikwazo  vya  silaha  dhidi  ya  viongozi  wa  wanamapinduzi wakishia wa Huthi  nchini  Yemen.

Baraza  hilo pia  limeweka  vikwazo  vya  kusafiri  pamoja  na kuzuwia  mali za  kiongozi  wa  wanamapinduzi wa kishia wa Huthi Abdul Malik al-Houthi.

Azimio  hilo limetoa  wito  kwa  makundi  yanayompinga rais Hadi nchini Yemen, hususan  kundi la Mashia la Huthi , kusitisha  ghasia  hizo  na  kuanza  tena haraka  majadiliano  yanayosimamiwa  na  Umoja  wa  Mataifa  ili kuwezesha  kipindi  cha  mpito  cha  kisiasa.

Azimio  hilo  liliwasilishwa  na  Jordan  jana  Jumanne na limeidhinishwa  na  nchi 14  katika  baraza  hilo  lenye  wajumbe  14.

Urusi , mshirika  wa  Iran  nchi  ambayo  inashutumiwa  kwa kuwaunga mkono Wahuthi, haikupiga  kura hiyo.

Weledi wa mambo wamestaajabishwa na kuwekwa vikwazo hivyo kwa wahuthi badala ya kuwekewa Saudia arabia ambayo imeivamia Yemen na kuishambulia kwa silaha nzito.