Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri mkuu wa Iraq alionana na rais wa Baraka Obama siku ya Jumanne, rais wa Marekani katika mazungumzo yake na waziri huyo amesema: si suala la ajabu kustawi mahusiano ya Baghdad na Teheran kutokana na kupakana na kuwiana kitamaduni na kijamii.
Aidha aliongeza kusema kuwa: asilimia kubwa ya wananchi wa Iraq ni wafuasi wa madhehebu ya shia ambapo hilo pia ni moja kati ya sababu zinazopekea kuwa na mafungamano mazuri na serikali ya jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Naye alisema umeundwa Muafaka wa kimataifa wakupambana na kikundi cha kigaidi cha Daesh kwaajili ya kuwa pamoja na Serikali ya Iraq, ama masuala hayo yote hayana athari yeyote mpaka serikali ya Iraq iwe na mpango mzuri wa kisiasa ambao utajumuisha wairaq wote kwa ujumla, kwa maana wairaqi wote mashia, masuni na wakurdi wawe kitu kimoja kwakufuata kauli moja ya serikali ya Baghdad nakuhusika katika kutoa maamuzi.
Obama alibainisha kuwa majeshi yote yanayotoka mataifa ya nje ya Iraq wanaoshiriki katika vita nchini dhidi ya magaidi wa Daesh wanapaswa kuiheshimu na kuitii serikali ya Iraq.
Haidar Alabadi waziri mkuu wa Iraq naye alisema: moja kati ya masuala muhimu ya safari hii ni kufanya mahusiano mazuri baina washiriki wa serikali ya Marekani kwaajili ya kukiondosha kikundi cha Daesh katika ardhi ya Iraq.
Aidha alisema kuukomboa mkoa wa Musil ambao mpaka sasa unamwaka mmoja unakaliwa na kikundi cha Daesh, nikatika mambo muhimu ya dharura kwa serikali ya Baghdad na baada ya kuukomboa mkoa huo utafuata mkoa wa Ambar na kumalizia mkoa wa Nainawa, ama suala muhimu ni kwamba katika harakati hizo zote tutakuwa pamoja na jeshi la kimataifa maalumu lakupambana na Daesh nchini Iraq.
Naye alimalizia kusema kuwa: jambo muhimu kwa serikali ya Baghdad kwa sasa ni kuikomboa ardhi yake mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
15 Aprili 2015 - 13:20
Msimbo wa Habari: 683921
Waziri mkuu wa Iraq Haidar Alabadiy katika safari yake nchini Marekani aonana na Rais Baraka Obama nakuzungumzia suala la kupambana na magaidi nchini Iraq