17 Aprili 2015 - 18:51
Obama kukutana na viongozi wa Ghuba

Rais wa Marekani, Barack Obama atakutana na viongozi wa Baraza la Ushirikiano la nchi za Ghuba, katika Ikulu ya Marekani Mei 13 mwaka huu na katika makazi ya rais Camp David, Maryland.

Rais wa Marekani, Barack Obama atakutana na viongozi wa Baraza la Ushirikiano la nchi za Ghuba, katika Ikulu ya Marekani Mei 13 mwaka huu na katika makazi ya rais Camp David, Maryland.

Ikulu ya Marekani imesema mkutano huo wa kilele utawajumuisha viongozi kutoka Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu. Mkutano huo utakuwa ni fursa kwa Rais Obama kuzungumzia wasiwasi kuhusu mpango uliofikiwa na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia pamoja na nafasi ya Marekani katika mashambulizi ya kijeshi dhidi ya raia wa Yemen, inayoendeshwa na nchi za Ghuba.