24 Februari 2016 - 18:14
Majeshi ya Syria yapata ushindi mpya katika mkoa wa Halab

Majeshi ya Syria yamefanikiwa kukikomboa kijiji muhimu kilichokuwa chini ya vikundi vya kigaidi katika mkoa wa Halab

Shirika la habari AhlulBaty (a.s) ABNA: majeshi ya nchi hiyo yamefikia ushindi huo kwa kukikomboa kijiji cha (Rasul Nafli) sehemu ya Humeh ya kusini katika mkoa wa Halab kutoka mikononi mwa magaidi wa kikundi cha Daesh.
Katika mashambulio hayo yaliofanywa na majeshi ya Syria makumi ya magaidi hao wameangamia katika mashambulio hayo na wengine kukimbia kijiji hicho, huku majeshi hayo yakiendeleza kufanya mashambulizi makali kwaajili ya kuukomboa mji wa (Hanasira) sehemu ambayo ni njia muhimu yakwenda Hanaswira nchini Syria.
mwisho wa Habari/290