16 Machi 2016 - 18:53
Wakurdi wa Syria kujitangazia utawala wa ndani

Vyama vya wakurdi wa Syria ambavyo vimekutana leo Kaskazini mwa Syria, vimetarajiwa kuunda utawala wa ndani katika maeneo wanayoyadhibiti.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Vyama vya wakurdi wa Syria ambavyo vimekutana leo Kaskazini mwa Syria, vimetarajiwa kuunda utawala wa ndani katika maeneo wanayoyadhibiti. Hatua hiyo ambayo inapanua mtindo wa utawala wa ndani uliopo sasa itatazamwa kwa wasiwasi mkubwa na Uturuki, ambayo inahofu kuwa wakurdi watajaribu kuimarisha uhuru wa maeneo yao.

Makundi ya wakurdi yanayoyadhibiti maeneo ya Kaskazini mwa Syria hayakujumuishwa katika mazungumzo ya amani yanayoendelea mjini Geneva. Wajumbe zaidi ya 150 kutoka vyama vya wakurdi, waarabu na makundi mengine wamekutana leo katika mji wa Rmeilan ulioko katika jimbo la Hasakeh Kaskazini Magharibi mwa Syria. Mshauri katika chama kikuu cha wakurdi wa Syria PYD Sihanuk Dibo amesema watajaribu kuafikiana juu ya uundwaji wa Shirikisho, na kuongeza kuwa uamuzi wa mwisho utajulikana kati ya leo na kesho.

Uturuki imekuwa ikilitumia kundi la kigaidi la Daesh kuwaua wapiganaji wa kikurdi sanjari na Marekani na Saudia arabia na washirika wao ambao wamekuwa wakilitumia kundi hilo kuangusha serikali ya Bashar asad wa Syria lakini mipango yao haikufanikiwa kutokana na Majeshi ya Iran na Urusi kuingilia kati na kutetea haki za wananchi naa kuilinda serikali halali ya Syria.

Mwisho wa habari / 291