18 Machi 2016 - 18:52
Kamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh afa nchini Syria

Mmoja kati ya makamanda wakuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria aangamia katika mkoa wa Halab

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari ya kuangamia kwa kamanda mwingine wa kikundi cha kigaidi cha Daesh imetangazwa nchini Syria.
(Hassan Abuudiy) ni miungoni mwa magaidi maarufu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mapambano na majeshi ya serikali ya Syria ambapo ameangamia katika mkoa wa Halab nchini humo.
Abuudiy ni mwanzilishi wa kikundi cha kigaidi cha (Liwau Daudi) ambapo miezi kadhaa iliopita kilijiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh naye kuwa miungoni mwa makamada wakuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria.
Kikundi cha kigaidi cha “Liwau Daudi” ndicho kilichohusika na mauaji ya (Ismail Haidariy) ambaye alikuwa ni kionguzi wa kikundi cha wapiganaji wanaoilinda Haram ya Bibi Zainab (a.s) pia kikundi cha Liwau Daudi kimehusika na mauaji ya “Hadiy Baghbaniy” mtengenezaji wa filamu aliokuwa katika midani ya vita katika eneo la Homah ya kusini katika mkoa wa Halab nchini Syria.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria katika wiki hizi za mwishoni kimepata mapigo makubwa kutoka kwa majeshi ya serikali ya Syria, ambapo majeshi ya Syria yamefanikiwa kukomboa eneo kubwa la sehemu ya Homeh ya mashariki na kusini mwa mkoa wa Halab na kuwasambaratisha magaidi wote waliokuwa katika maeneo hayo.
mwisho wa Habari/290